Simba SC yatangaza kocha mkuu

Klabu ya Simba imemtangaza Roberto Oliveira kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Zoran Maki aliyetimuliwa miezi kadhaa iliyopita.

Kocha huyo amejiunga Simba akitokea Vipers ya nchini Uganda ikiwa ni wiki moja tangu alipoachana na timu hiyo kwa kuvunja mkataba baada ya taarifa za kupokea ofa kutoka Simba.

Oliveira sasa ataungana na aliyekuwa kaimu kocha wa timu hiyo, Juma Mgunda ambaye atakuwa kocha msaidizi sambamba na Suleiman Mataola katika benchi la ufundi.

Habari Zifananazo

Back to top button