Simba SC yatangaza tarehe ya uchaguzi

Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba leo November 26, 2022 imetangaza tarehe ya uchaguzi wa klabu hiyo kuwa ni 29 January 2023.

Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni mwenyekiti, na Wajumbe watano wa bodi ya wakurugenzi. Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litaanza Disemba 5 hadi 19 katika ofisi za klabu hiyo zilizopo Masaki Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kamati hiyo, Boniface Lyamwike ametaja kigezo cha yoyote anaeutaka uenyekiti wa Simba lazima awe na shahada.

“Mtu yoyote ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ni lazima awe na angalau shahada ya Chuo Kikuu na lazima awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha klabu ndani na nje ya nchi” amesema Lyamwike

Ametaja kigezo kingine cha mgombea nafasi ya ujumbe wa bodi kuwa ni lazima awe amefika kidato cha nne na cheti za kuhitimu, kigezo kingine awe mzoefu wa angalau miaka mitatu ya uongozi wa soka.

“Kingine asiwe amepatikana kamwe ya hatia ya kosa ya jinai, lakini pia angalau awe na miaka 25 na si zaidi ya miaka 64, lakini pia asiwe mmiliki, mwanahisa au kiongozi wa timu nyingine ya mpira wa miguu.

” ameongeza.

Habari Zifananazo

Back to top button