Simba, Singida kazi ipo leo

 

SIMBA SC leo itakuwa na kibarua kingine cha kutafuta alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars mchezo utakaopigwa saa 10 jioni Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Wawili ho wanaingia katika mchezo huo wakiwa na pointi 17, tofauti ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa, Simba ikiwa nafasi ya pili wakishinda michezo miwili ya mwisho na Singida nafasi ya nne ikiwa imepoteza michezo miwili ya mwisho.

Pigo kwa Simba kuelekea mchezo huo, itakosa huduma ya kiungo wao, Clatous Chama ambaye amefungiwa michezo mitatu na Bodi ya Ligi kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika Oktoba 23,2022.

Kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda ameguswa na adhabu iliyotolewa Chama kiasi cha kuharibu mipango yao kuelekea mchezo huo.

Wao walikuwa wanajua, wameamua tangu Ijumaa saa nne, ni haki yao kabisa, lakini ningeomba tu na kuwashauri, linapotokea jambo kama hili basi waliseme tu mapema, ili tuendelee na mipango mingine,” ameeleza Mgunda.

 

Habari Zifananazo

Back to top button