Simba waifuata Mashujaa Kigoma
DAR ES SALAAM; Kikosi cha timu ya Simba kinaondoka Dar es Salaam mchana huu kwa ndege kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Mashujaa ya huko utakaochezwa kesho Uwanja wa Lake Tanganyika.
–
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema, baada ya kutolewa hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-0 na Al Ahly ya Misri, sasa wanahamishia nguvu zao katika mashindano ya ndani.
Simba Ijumaa ilifungwa mabao 2-0 na Al Ahly mjini Cairo, Misri katika mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo kutupwa nje ya michuano hiyo baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Simba kupoteza kwa bao 1-0.