Simba waigeukia Wydad

Kocha Juma Mgunda

KIKOSI cha Simba kinaingia kambini jioni ya leo kujiandaa na mchezo wa robo fainali wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca,  utakaopigwa Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Akizungumza na HabariLEO,  Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Juma Mgunda amesema mikakati yao ni kuzitumia siku zilizobaki kuwapa wachezaji wao mbinu muhimu zitakazowapa ushindi mnono utakaowavusha hatua ya nusu fainali.

“Ni mchezo mgumu sababu tunakutana na mabingwa watetezi, lakini hata sisi siyo wanyonge tutazitumia siku zilizobaki kuhakikisha tunamaliza mchezo hapa nyumbani kwa kupata ushindi mnono, ili tusiwe na kazi ngumu kwenye mchezo wa marudiano,” amesema Mgunda.

Advertisement