Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa leo Februari 26, 2023 ameikabidhi timu ya Simba Sc Sh milioni 5 ikiwa ni ahadi ya Rais Samia Suluhu ya kutoa milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa na Simba au Yanga katika michuano ya kimataifa.
Simba SC wamekabidhiwa fedha hizo baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers katika mchezo wa raundi ya tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mpaka sasa Simba imepata milioni tano katika michezo miwili badaa ya kufunga bao moja, wakati watani wao Yanga wamevuna milioni 15 baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.
Yanga inacheza na Real Bamako katika mchezo wa kombe la Shirikisho utakaofanyika nchini Mali leo saa 1:00 usiku.