Simba wakitaka lao raha sana!

SIMBA wakitaka lao raha sana, Simba ndiyo zao kimataifa, pengine hivyo ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa wa leo kati ya Simba na Horoya Ligi ya Mabingwa Afrika uliomalizika muda mfupi uliopita Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 7.0.

Ni matokeo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa na mashaabiki wa timu hiyo, matokeo yaliyoiwezesha Simba kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufikisha pointi tisa katika kundi lao, pointi ambazo ukiacha Raja Cassablanca iliyozivuka ikiwa na pointi 13 hakuna timu nyingine katika kundi hilo yenye uwezo wa kuzifikia.

 

Simba inaendelea kubaki nafasi ya pili katika kundi hilo ikiwa na pointi 9, wakati Horona imesalia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4. Vipers ni ya mwisho ikiwa na pointi mbili.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yamefumgwa na Clatous Chama aliyefunga mabao matatu, Jean Baleke na Sadio Kanoute ambao kila mmoja amefunga mabao mawili.

Habari Zifananazo

Back to top button