Simba wamfukuza kocha
KLABU ya Simba ya Dar es Salaam, imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Zoran Maki.
Taarifa kwa umma iliyotolewa muda mfupi uliopita na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, imesema uamuzi huo umefikiwa kwa makubaliano ya pande zote mbili na kwamba timu hiyo kwa sasa itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Suleiman Matola.