Simba wapania makubwa kesho

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amesema mchezo wa kesho dhidi ya Wydad Casablanca utakuwa mgumu, lakini matumaini ya ushindi ni makubwa kutokana mikakati yao na utayari waliokuwa nao wachezaji wake.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari Uwanja wa Benjamin Mkapa, kocha huyo amekiri kuwa wapinzani wao Wydad ni timu bora na kubwa Afrika, lakini hilo haliwapi presha sababu siku zote mechi za michuano hiyo hazijawahi kuwa rahisi na uzuri wapo nyumbani mbele ya mashabiki wao.

“Kwangu nafurahi kucheza na Wydad ni timu mgumu nakubali, lakini tuna mikakati yetu ambayo tumeiandaa kwa ajili ya mchezo huo, lengo letu ni kucheza kwa kushambulia na kuzuia kwa pamoja lakini pia tunataka kufunga mabao mengi ili kuumaliza mchezo hapa nyumbani,” amesema Robertinho.

Kwa upande wake beki Shomari Kapombe amesema mchezo huo wa kesho wamepanga kuonesha walichokuwa nacho na kuthibitisha ubora wa Simba hasa wanapokuwa nyumbani mbele ya mashabiki wao, ambao wamekuwa na msaada mkubwa kwao.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button