Simba wapo imara Morocco

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amesema wapo tayari kuikabili Wydad Casablanca kesho na kwa maandalizi waliyofanya anaamini watapata ushindi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha huyo amesema yeye na wachezaji wake wanajua ugumu wa mchezo huo, lakini wapo kwa ajili ya kuipigania Simba na Tanzania na hilo litaonekana baada ya dakika 90 za mchezo huo.

“Watu wengi hawatupi nafasi ya kuitoa Wydad sababu wao ni timu kubwa na inacheza nyumbani, lakini Simba inaweza kushinda popote tumefanya hivyo kwenye hatua zilizopita na kesho tutaishangaza Afrika kwa kuwatoa mabingwa watetezi kwao,” amesema Robertinho.

Miamba hiyo ya Tanzania inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote itakuwa imeingia Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button