Simba wapo tayari kwa vita kesho

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema wapo tayari kuikabili Raja Casablanca kesho kutokana na maandalizi waliyofanya na utayari wa wachezaji wao.

Akizungumza Dares Salaam leo, kocha huyo amesema lengo lao kubwa nipointi tatu ambazo zitawaweka katika nafasi mzuri kwenye msimamo wa kundi C.

“Naiheshimu Raja Casablanca ni timu mzuri na bora, lakini hata Simba ni timu kubwa na ndio maana tupo wote katika hatua hii kitu cha msingi kwetu ni kupata pointi tatu na kutoa burudani kwa mashabiki wetu watakao uja uwanjani kutuunga mkono,” amesema.

Huo ni mchezo wa kwanza nyumbani hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa Simba, ambapo mchezo wa kwanza wa michuano hiyo wiki iliyopita ilifungwa bao 1-0 na Horoya AC nchini Guinea.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x