Simba watakiwa kutanguliza mbele maslahi ya klabu

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewataka wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Simba kutanguliza mbele maslahi ya timu hiyo na kuacha kumuangalia mtu.

Akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Dar es Salaam, kiongozi huyo ameeleza kuwa ni vyema watu wakashindana kwa hoja na kufikiria kuifikisha mbali klabu hiyo, ikiwemo na kujenga miundombinu imara ya kujitegemea.

“Naamini mmekuja kutimiza jukumu la kikatiba, hivyo ni vyema kila mmoja akatanguliza maslahi ya klabu hii mbele, Simba ni timu iliyojipambanua kiushindani zaidi hilo linapaswa kuendelea na kufika mbali zaidi ya ilivyo sasa,” amesema Makalla.

Kiongozi huyo pia amewapongeza wanachama na viongozi wa klabu hiyo kwa kumpata Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), Iman Kajula kwa sababu ni mtu wa mpira.

Habari Zifananazo

Back to top button