Simba watemana na Phiri, Baleke
Simba SC imetangaza kuachana na Washambuliaji wake wawili Jean Baleke na Moses Phiri.
Klabu hiyo imetoa taarifa za kuachana na wachezaji hao leo kupitia mitandao yao ya kijamii.
Mapema leo Simba ilitangaza pia kuachana na wachezaji wanne kwa mpigo baada ya kutoridhishwa na viwango vyao akiwemo Mohamed Mussa, Shaban Chilunda, Nassor Kapama pamoja na Jimmyson Mwanuke.
Simba tayari imeshasajili wachezaji wawili katika dirisha dogo la usajili.