Simba SC watoa pole waathirika mafuriko Hanang

KLABU ya Simba SC imetoa pole kwa familia zilizoguswa zilizopoteza ndugu zao katika mafuriko yaliyotokea Wilaya ya Hanang mkoani Manyara jana.

“Simba inaungana na Watanzania wote kuomboleza vifo vya wenzetu waliotangulia pamoja na kuwaombea majeruhi wapone haraka.” Imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana wilayani humo yamesababisha vifo vya watu 47 na kujeruhi 85.

Sambamba na hilo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Disemba 4, 2023 ameelekea katika Mji wa Kateshi, ulioko wilayani Hanang kuwajulia hali waathirika wa mafuriko yaliyoambatana na maporomoko ya udongo.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button