Simba, Wydad kupigwa saa 4 usiku

MCHEZO wa Ligi ya Mabingwa kati ya Simba SC dhidi ya Wydad utapigwa saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania, ambapo itakuwa saa 2:00 kwa saa za Morocco.

Simba SC wamethibitisha taarifa hiyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Mchezo huo wa marudiano utapigwa kesho katika Uwanja wa ‘Mohammed V’. Awali mchezo huo ulipangwa kupigwa saa 3 usiku.

Simba wataingia katika mchezo huo wakiwa na faida ya goli 1 walilopata katika mchezo wa raundi ya kwanza, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button