Simba yaagana na Sakho

KLABU ya Simba imefikia makubaliano ya kumuuza kiungo mshambuliaji Pape Sakho kwenda klabu ya Quevilly Rouen Metropole.

Simba imetoa taarifa hiyo leo Julai 24, 2023 kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

“Tunamtakia kila la kheri Sakho kwenye timu yake mpya” imeeleza taarifa hiyo.

Simba ilimsajili Sakho Agosti 14, 2021 akitokea Tungueth Rufisque ya nchini Senegal.

Habari Zifananazo

Back to top button