Simba yaangukia pua Cairo

CAIRO, Misri: SIMBA ya Dar es Salaam imeyaaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Matokeo haya yanaifanya Simba kupoteza nje na ndani katika hatua ya Robo Fainali kwa jumla ya mabao 3-0.

Kabla ya mchezo huo, tumaini pekee la Tanzania katika CAFCL lilikuwa kwa Simba SC baada ya mapacha wao Yanga SC kutolewa mapema katika hatua hiyo kwa changamoto ya mikwaju 3-2 jijini Pretoria dhidi ya Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini.

Habari Zifananazo

Back to top button