Simba yafufukia Unguja
UNGUJA, Zanzibar: BAADA ya ukame wa michezo minne pasi na ushindi, mnyama @simbasctanzania leo, Aprili 24, 2024 amefufuka kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ, katika michuano maalumu ya Kombe la Muungano ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.
–
Dakika 25′ zimetosha kwa Freddy Koublan kuwainua vitini mashabiki wa mnyama Simba katika Uwanja wa New Amaan complex, visiwani Unguja, Zanzibar.
Dakika 90’+4 Israel Mwenda anaihakikishia Simba kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ikiwa ni marejeo ya baada ya kufanyika miaka 20 iliyopita.
Nusu fainali ya pili itachezwa kesho, Azam FC watakapokabiliana na KMKM majira ya saa 2:15 usiku.
Kombe la Muungano linaratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) na ndugu zao Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).