Simba yafuzu makundi Afrika

Simba kujipima na CSKA Moscow 

SIMBA imefuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa ya Mabingwa Afrika, baada ya jioni hii kuifunga Primiero de Agosto ya Angola bao 1-0 Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, ikiwa ni mchezo wa marudiano.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Uwanja wa Novemba 11 mjini Luanda nchini Angola na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 1-3, hivyo kwa ushindi wa leo imeingia hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-1. Bao pekee katika mchezo wa leo lilifungwa na raia wa Zambia Mosses Phiri kipindi cha kwanza.

Advertisement