Simba yakabidhi msaada waathirika Hanang

DAR ES SALAAM; Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro leo Desemba 5, 2023 jijini Dar es Salaam amepokea vitu mbalimbali ikiwemo vyakula, sukari, sabuni, unga wa ngano na maji kutoka klabu ya Simba ikiwa ni msaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Dk Ndumbaro ameipongeza klabu ya Simba kwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa msaada huo, ambao unaenda kusaidia waathirika hao.
Dk Ndumbaro amezitaka klabu nyingine nchini kuiga mfano wa Simba kwa kutoa msaada kwa jamii ya wananchi wa Hanang kutokana na mafuriko yaliyowakumba usiku wa kuamkia Desemba 3, 2023.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button