Simba SC imethibitisha kumtoa kwa mkopo beki Joash Onyango (30) kwenda Singida Fountain Gate FC.
Uongozi wa Simba SC umetoa taarifa hiyo leo Julai 8, 2023 na kwamba mkopo huo utafika mwisho msimu wa 2023/2024.
Mkataba wa Onyango umesaliwa mwaka mmoja Simba SC, hivyo baada ya msimu kumalizika mchezaji huyo atakuwa huru na atakuwa amemalizana na klabu hiyo.