Simba yamtambulisha Onana kutoka Rwanda

KLABU ya Simba imekamilisha usajili wa mshambuliaji, Willy Essomba Onana, 23, raia wa Cameroon akitokea Rayon Sports ya Rwanda.

Onana amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Rwanda akiwa na magoli 16 na pasi za mabao 5.

Msimu uliopita Onana alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu nchini humo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button