Simba yatambulisha skauti
KLABU ya Simba imemtangaza Mels Daalder kuwa Mkuu wa ‘Skauti’ katika benchi la ufundi la timu hiyo lililo chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’.
Mels raia wa Uholanzi ametangazwa kupewa wadhifa huo jana ikiwa zimepita siku mbili tangu Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally kutangaza kuwa wako mbioni kukamilisha mchakato wa kumsaka mtaalam wa masuala hayo.
Mels ni raia wa Uholanzi mwenye uzoefu wa kufanya skaauti katika timu mbalimbali ikiwemo Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu ya EPL.
Mels ameshiriki kozi mbalimbali za scouting duniani ikiwa ni pamoja na kozi zikizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.
mwisho.