Simba yanasa kipa Mbrazil
- UNAWEZA kusema sasa Aishi Manula atakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha anaendelea kudumu golini, baada ya leo Simba SC kukamilisha uhamisho wa kipa Jefferson Luis kutoka Brazil.
–
Leo Julai 23, 2023 Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa Luis kwa mkataba wa miaka miwili.
–
Jefferson (29) anaenda kukutana na ushindani pia kutoka kwa Manula na kipa namba tatu Ally Salim.
–
Usajili huo ni mwendelezo wa Simba SC kujiweka sawa kwa ajili ya michuano ya kimataifa.