ZANZIBAR: MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2024, Mbarouk Othman ametangaza makundi ya timu zitakazoshiriki Mashindano ya Kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar.
Akiwa visiwani Zanzibar, Othman amesema mashindano ya mwaka huu yatakuwa katika mgawanyo wa makundi matatu, A, B na C.
Kundi-A litahusisha vilabu vya Mlandege FC, Azam FC, Chipukizi United SC, URA FC ya Uganda.
Kundi-B likijumuisha timu ya Simba SC, Jamhuri SC, APR SC ya Rwanda na Singida Fountain Gate.
Na Kundi-C likiwa na timu ya Yanga SC, Bandari SC ya Kenya, KVZ FC, na Vital’o SC ya Burundi.
“Mashindano yetu yataanza Desemba 28, 2023 na kutamatika Januari 13, 2024 huku yakijumuisha timu 12,” amesema mwenyekiti huyo.
Mashindano ya Mapinduzi ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar, yaliyoondoa madarakani Utawala wa Sultan mnamo Januari 12, 1964.
Comments are closed.