BAADA ya kuanza vibaya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake timu za soka za Simba na Yanga leo zimezinduka baada ya kupata ushindi mnono katika mechi zao za mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Mabingwa watetezi Simba leo walikuwa ugenini mkoani Arusha na wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tigers Queens katika mchezo ambao umepigwa uwanja wa Black Rhino Karatu
Mabao ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Opah Clement aliyefunga mabao mawili katika dakika za 2 na 68 na Pambani Kuzoya naye amefunga idadi kama hiyo ya mabao dakika za 48 na 52
Katika mchezo mwingi uliofanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Yanga Princess nayo imetoa kichapo kikali cha mabao 4-0 dhidi ya wageni Mkwawa Queens
Mabao ya Yanga Princess yamefungwa na Success Wogu , Aniela , Blessing Nkor na Precious Christopher huo ukiwa ni ushindi wa kwanza chini ya kocha Sebastian Nkoma aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akichukua nafasi ya Edna Lema aliyefutwa kazi.
Timu hizo mbili zilianza vibaya msimu huu baada ya kupoteza michezo yao ya ufunguzi Simba ikifungwa mabao 2-1 na JKT Queens na Yanga ikakubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Fountaingate