Simba yaondolewa Caf kwa penalti

SAFARI ya Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2022/23 imeishia robo fainali baada ya kupoteza kwa penati 4-3 dhidi ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco.

Dakika 90 za mchezo wa raundi ya pili wa hatua hiyo ziliwapa wenyeji ushindi wa bao 1-0 likifungwa na mshambuliaji BoulySambou, hivyo matokeo kuwa 1-1 kwa kuwa Simba ilishinda katika mchezo wa kwanza 1-0.

Wydad itacheza na timu itakayosonga mbele kati ya CRBelouizdad ya Algeria au MamelodiSundowns ya Afrika Kusini.

Advertisement

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *