Simba yapangwa na Wamorocco

TIMU ya Simba ya Dar es Salaam imepangwa Kundi C la michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Simba ambayo msimu uliopita ilifikia Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), ipo kundi moja na timu ya Vipers SC ya Uganda, Horoya AC ya Guinea na Raja Casablanca ya Morocco.

Kwa mujibu wa droo iliyochezeshwa leo Jumatatu Desemba 12, 2022, Kundi A lina mabingwa watetezi, Wydad Athletic ya Morocco, Petro Atletico ya Angola na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Timu za Kundi B ni  Al Ahly ya Misri, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, El Hilal ya Sudan na Cotón Sport ya Cameroon, huku Kundi D likiwa na timu za Esperance ya Tunisia, Zamalek ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria na El Merreikh ya Sudan.

Habari Zifananazo

Back to top button