Simba yasaini mkataba utengenezaji jezi

KLABU ya Simba wameingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh bilioni 2 kwa kila mwaka na kampuni ya Sandaland kwa ajili ya udhamini wa utengenezaji na usambazaji wa jezi za msimu wa 2023/24.

Akiongea katika hafla ya utiaji saini ya mkataba huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba (CEO) Imani Kajula amesema ili wawe timu bora ni lazima wawe na uwezo wa kifedha na hilo ndilo wanalolisimamia.

“Mwanzoni tulikuwa tunapata milioni 400 kwa mwaka kutokana na jezi. Akaja vunja bei akatupa bilioni moja kwa mwaka na huyu wa sasa anakuja kutupa bilioni mbili kwa mwaka.” CEO Kajula

Advertisement

Hata hivyo, ameongeza kuwa mkataba huu ni sehemu ya kutekeleza kilio cha mashabiki wao kilichodai jezi bora kwa wakati sahihi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *