TIMU ya soka ya Simba ya Dar es Salaam, imetoka sare ya mabao 2-2 na CSKA Moscow ya Urusi mchezo uliomalizika muda mfupi uliopita mjini Abu Dhabi.
Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki uliokuwa mkali na wa kusisimua, ambapo hadi mapumziko Simba ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0.
Hata hivyo Simba ilibadilika kipindi cha pili na kusawazisha mabao hayo mfungaji akiwa Habib Kyombo. CSKA inashiriki Ligi Kuu ya Urusi.