Simiyu yaongoza kwa utegemezi

DAR ES SALAAM: Tanzania ina idadi kubwa ya wategemezi ambapo kati ya watu 100 watu 87 wanauwezo wa kufanya kazi lakini hawajishughulishi huku mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiongoza.

Hiyo ni kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 ambapo imebaini Simiyu inaongoza kwa kuwa na wategemezi 119 ukifuatiwa na Tabora na Katavi 110 kila moja.

Mkoa wa Dar es Salaam umetajwa kuwa na uwiano mdogo wa wategemezi ambao ni 51.

Akizungumza Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Omari Mdoka leo Machi 13, 2024 amesema takwimu zinaonyesha kuwa wenye umri wa miaka 15 hadi 64 ni tegemezi.

Akitoa mchanganuo wa takwimu hizo, Mdoka amesema katika sensa ya mwaka 2022 mbali na Simiyu, Tabora na Katavi pia mikoa mingine ni Kigoma wategemezi 109, Rukwa 109, Mara 107, Geita 107 na Singida 105.

Habari Zifananazo

Back to top button