Simon Harris Waziri Mkuu  Ireland

DUBLIN, IRELAND: BUNGE la Ireland limemchagua Simon Harris kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.

Harris anakuwa Waziri Mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchini humo.

Simon anachukua nafasi ya Leo Varadkar kufuatia kujiuzulu kwake mwezi uliopita jambo ambalo liliwashangaza wengi nchini Ireland.

Wakati wa kuchaguliwa kwake wabunge walilipuka kwa shangwe kubwa ya uthibitisho wa 88-69, baada ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya wabunge huru, pamoja na washirika wake wa muungano wa Fianna Fail na Green Party.

Waziri wa zamani wa afya na elimu ya juu mwenye umri wa miaka 37, anayejulikana sana kwa kusaidia kukabiliana na Ireland katika janga la COVID-19, alichaguliwa bila kupingwa kama kiongozi mpya wa chama cha mrengo wa kulia cha Fine Gael mwezi uliopita.

“Ninakubali uteuzi huu kuhudumu nafasi ya Waziri Mkuu,” Harris amesema. Ninajitolea kufanya kila niwezalo kuiheshimu imani ambayo mumeiweka kwangu, nitajitahidi kuongeza umoja wa ushirikiano na kuheshimiana.

“Nitakuza maadili ya msingi, kama vile biashara, kilimo na sheria pamoja na utaratibu wa nchi,” alisema Harris.

Kuchaguliwa kwa Harris kama waziri mkuu kunapunguza ombwe la ongezeko la kisiasa lilikuwepo kwa muda nchini humo.

Harris alijiunga na tawi la vijana la Fine Gael akiwa na umri wa miaka 16 na akapanda vyeo haraka akawa diwani wa eneo hilo akiwa na umri wa miaka 22, alichaguliwa kuwa mbunge akiwa na umri wa miaka 24 mwaka wa 2011. Wakati huo alikuwa mbunge mdogo zaidi na alipewa jina la utani “Baby of the Dail” (bunge la Ireland).

Habari Zifananazo

Back to top button