Singida Big Day Agosti 2, 2023
SINGIDA Fountain Gate wametangaza Agosti 2, 2023 kuwa ni siku ya tamasha lao la Singida Big Day litakalofanyika uwanja wa Liti mjini Singida.
Kupitia tamasha hilo SFG itatambulisha kikosi chake chote kitakachotumika msimu wa 2023/24 pamoja na kucheza mechi ya kirafiki.
SFG haijaweka wazi timu itakayocheza nayo katika tamasha hilo.