Singida FG wameamua kuanza upya

MWANZA: Uongozi wa klabu ya SINGIDA Fountain Gate FC umetangaza kumfuta kazi kocha, Thebo Senong na benchi lake zima kufuatia mwendelezo wa matokeo mabaya ya timu hiyo ambayo kwasasa imeweka makazi yake jijini Mwanza.

Kocha Thebo alikabidhiwa kibarua cha kukinoa kikosi hicho akipandishwa kutoka kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo baada ya kuondoka kwa kocha Ricardo Ferreira ambapo alianza majukumu  mwezi Januari mwaka huu, huku Nizar Khalfan akiteuliwa kuwa kocha msaidizi ambaye awali alikuwa meneja wa timu hiyo.

Chini ya kocha Thebo katika mechi tano za Ligi kuu alizoiongoza timu hiyo amepoteza michezo minne na kutoa sare mchezo mmoja.

Advertisement

Hata hivyo timu hiyo kwasasa inashika nafasi ya 11 baada ya michezo 19 ikiwa imekusanya alama 21. Mchezo unaofuata Singida FG itavaana na Simba Machi 12 mwaka huu.

Taarifa ya Singida imeeleza kuwa kocha mpya wa kikosi hicho atatangazwa muda wowote.