TIMU ya Singida Big Stars, imetamba itabeba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kutokana na ubora wa kikosi chao.
“Tunajivunia rekodi nzuri katika mechi zilizopita tangu hatua ya makundi tumetoka sare na Yanga na tumeifunga Azam FC mabao 4-1 kwenye hatua ya Nusu Fainali,”amesema Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm.
Pluijm ameeleza kuwa pamoja na ubora wa kikosi chake, lakini wanawaheshimu wapinzani wao Mlandege kutokana na kiwango walichokionesha mechi zilizopita.