Singida yafungiwa usajili

KLABU ya Singida Fountain Gate FC, imefungiwa usajili mpaka itakapokamilisha malipo ya mchezaji Rodrigo Carvalho.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) leo imeeleza kuwa taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA).

Mchezaji huyo raia wa Brazil alifungua kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo na baada ya kushinda ndipo hukumu hiyo imepita.

Singida ilipewa siku 45 kutekeleza hukumu hiyo, hata hivyo ilishindwa kufanya hivyo.

Wakati FIFA ikitoa adhabu hiyo, TFF pia imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji wa ndani.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button