Siri ya ‘mafanikio’ soko la viazi Urafiki yatajwa

MSIMU wa ufungaji wa vyuo vikuu mkoani Dar es Salaam unapunguza ununuaji wa viazi katika soko la Urafiki.

Hali hiyo inathibitisha kwamba walaji wakubwa wa bidhaa hiyo ni wanafunzi wa vyuo vikuu.

Mfanyabiashara wa muda mrefu wa viazi katika soko hilo, George Nyangachi alisema hayo alipozungumza na HabariLEO.

“Walaji wakubwa ni wanafunzi wa chuo kwa sababu vyuo vikifungwa biashara zetu zinadorora, wakifungua wanafunzi wa chuo ni walaji wazuri wa chipsi,” alisema na kuongeza kuwa viazi katika soko hilo vinatoka mikoa ya Mbeya, Njombe, Kilimanjaro na nchini Kenya.

Alisema kwa kiasi kikubwa viazi vinatoka mkoa wa Njombe na Mbeya na vinavyotoka nchini Kenya vinaanza Julai hadi Septemba na kuwa kwa wastani kwa siku zinaingia gari 20 ambazo ni sawa na tani 400.

“Msimu huu tuna uwezo wa kuuza gari 15 kwa siku, lakini biashara zikichanganya viazi vinakuwa havitoshelezi.

Miezi ya Novemba hadi Mei, viazi vinauzwa kati ya Sh 60,000 hadi 100,000 kutokana na hali ya hewa. Lakini sasa gunia moja ni kuanzia Sh 50,000 hadi Sh 55,000,” alisema.

Alisema soko hilo linahudumia Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Zanzibar. Masoko mengine yanayouza viazi mkoani Dar es Salaam ni Temeke, Ilala na Mbagala.

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button