Small Jobiso kuja na bendi ya Singeli

MTAYARISHAJI wa muziki, mwanamuziki na mmiliki wa studio ya A Sound, Steven Joseph maarufu Small Jobiso amesema yupo katika harakati za kuanzisha bendi itakayokuwa ikipiga muziki wa singeli.

Small Jobiso ambaye sasa anajiita Dragon amesema amepanga kuanzisha bendi hiyo kwa sababu muziki wa singeli kwa sasa kibiashara upo vizuri unapendwa na una mashabiki wengi.

“Muziki wa singeli kwa sasa unalipa kuna mambo machache ya kubadilisha ambayo ni ya wasanii ili waondokane na dhana kwamba wanaoimba muziki huo ni wahuni na watu wasio na malengo” anasema Small Jobiso.

Advertisement

Ameongeza kuwa  bendi hiyo itawaonyesha wasanii kwamba lazima msanii wa singeli awe na mipango kama hawezi atafute wenye uwezo wamsimamie kufikia mafanikio kwa kupata shoo ndani na nje ya nchi lakini pia kupata ubalozi kwenye makampuni ya kibiashara.

Small Jobiso kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Dalali’ pia ameandika nyimbo za wasanii wengi ukiwemo wimbo wa ‘Walimwengu’ wa Sam wa ukweli.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *