Soko la karafuu kimataifa ni uhakika

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema serikali kupitia balozi zake na majukwaa mbalimbali yataendelea na jitihada za kufungua masoko ya zao la karafuu ili kuongeza uuzaji wa zao hilo nje ya nchi.

Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na wananchi katika tukio la azinduzi wa jengo la Kitega Uchumi la Zanzibar State Trade Cooperation – Pemba visiwani Zanzibar.

Rais Samia amesema mahitaji ya soko la karafuu kimataifa bado kubwa, hivyo amewataka wahusika wa uzalishaji wa zao hilo kuongeza jitihada katika uzalishaji wa zao hilo. Amesema wakati taifa linalenga kuongeza kiwango cha uzalishaji, shabaha ibaki katika kuongeza tija ya uzalishaji kwa kila ekari.

“Angalizo langu kwenye hili, tunapotafuta njia za kisanyansi kuongeza tija ya uzalishaji tusishushe hadhi na ubora wa karufuu yetu. Tuongeze uzalishaji lakini ubora wa karufuu yetu ibaki vile vile, tunaweza tukapata watalamu wa sayansi wakatuongezea uzalishaji lakini hadhi ya karufuu yetu ikashuka”.Amesema Rais Samia.

Habari Zifananazo

Back to top button