Soko la Kariakoo kukamilika Oktoba

UJENZI wa soko la Kariakoo linataraijwa kukamilika Oktoba mwaka huu 2023.

Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angela Kairuki amesema soko hilo litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 2,300 sawa na ongezeko la wafanyabishara 638 ukilinganisha na wafanyabiashara 1,662 waliokuwepo kabla ya ukarabati wa jengo la zamani na ujenzi wa jengo jipya.

Advertisement

Amesema, katika Mwaka wa Fedha wa 2022/23 jumla ya Shilingi Bilioni 10 ziliidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kariakoo unaohusisha ujenzi wa jengo jipya na Ukarabati wa Jengo la Soko la zmani.

“Hadi Februari, 2023 Shilingi Bilioni 4.

16 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu, sawa na asilimia 42 ya fedha zilizoidhinishwa.”Amesema Kairuki

Amesema, ujenzi wa soko hilo umefikia hatua ya kumwaga jamvi la ghorofa ya tano kati ya ghorofa sita ikihusisha ghorofa mbili za chini ya ardhi (basement).

Aidha, amesema ukarabati wa jengo la zamani unaendelea na umefikia asilimia 62.

144.

Amesema, kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa soko hilo utachochea ukuaji wa biashara katika Jiji la Dar es Salaam, mikoa mingine na nchi jirani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *