Soko la Machinga Tanga kugharimu Sh bil 7.7

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga inatarajia kutumia kiasi cha Sh bil 7.7 kwa ajili ya kujenga soko la kudumu ambalo litatumika na wafanyabiashara wadogo maarufu machinga.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko hilo, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa amesema kuwa kukamilika kwa soko hilo kutawasaidia wafanyabiashara hao kuwa na uhakika wa eneo ambalo wataweza kufanya shughuli zao kila siku.

“Tuna takribani wamachinga 900 ambao kwa sasa wanafanya shughuli zao kwa siku maalumu katika eneo ambalo sio rasmi la Tangamano lakini hapa sasa watakuwa na soko rasmi”alisema Mgandilwa.

 

Hata hivyo Mkurungenzi wa Jiji la Tanga, Sipora Liana amesema kuwa soko hilo litajengwa kwa kupitia fedha kutoka serikali kuu pamoja na mapato ya ndani .

Amesema kuwa soko hilo litakapokamilika wamachinga katika Jiji la Tanga wataweza kuwa na eneo lao rasmi kwa ajili ya kuuza bidhaa zao na hivy

Habari Zifananazo

Back to top button