Soko la mbaazi uhakika India

TANZANIA imepata soko la uhakiza la zao la mbaazi nchini India kwa mgawo wa tani laki mbili huku ikielezwa kuwa India ni mtumiaji mkubwa wa mbaazi duniani.
–
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Hatua hiyo imetokana na ziara iliyofanywa na Rais Samia nchini humo. Malawi na Msumbiji pia ni miongoni mwa waliopita fursa hiyo.
–
Aidha, Tanzania imewasilisha mahitaji kwenye serikali ya India, kupitia Exim Bank ya India kwa ajili ya mradi mkubwa wa umwagiliaji kutoka Ziwa Victoria.
–
Mahitaji hayo ni takribani Dola bilioni 1 ambao mradi huo utatekelezwa mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida, Dodoma, Kagera na Mara.
–
Pia Tanzania ina mpango wa kununua jumla ya trekta 10,000 na kujenga vituo maalum vya vifaa vya kilimo ‘mechanization’.
–
Serikali imekubaliana na kampuni kubwa mbili duniani ya matrekta, Mahindra na John Deer kuweka katika kipindi cha miezi 12 viwanda vya kuunganisha matrekta na kutengeneza vipuri ndani ya Tanzania.