WAKATI Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kikijiandaa kujiondoa mwishoni mwa 2024, Serikali ya Somalia inapanga kuchukua nafasi hiyo kwa kutafuta wanajeshi wa kigeni ili kuhakikisha usalama wa nchi hiyo unaimarika tena.
Taarifa ya Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Hussein Ali imeeleza kuwa Serikali inaandaa mpango unaoelezea idadi, majukumu, na chimbuko la vikosi hivi mbadala.
Amesema malengo muhimu ni pamoja na kulinda maeneo muhimu katika mji mkuu, Mogadishu, na kulinda balozi za kigeni, imeelezwa wanajeshi hao hawatashiriki katika vita dhidi ya kundi la wanamgambo la Al-Shabaab.
Nguvu inayotarajiwa ya askari ni kati ya 3,000 hadi 8,000, na muda uliopangwa wa kupelekwa ni mwaka mmoja.