Somo la maadili kutatua changamoto ya rushwa

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geofrey Pinda amewaagiza wakuu wa wyuo vya ardhi vya Morogoro na Tabora kuhakikisha somo la maadili linafundishwa kwa wanafunzi wa vyuo hivyo ili hapo baadae waweze kukabiliana na changamoto ya rushwa iliyogubika sekta ya ardhi nchini.

Akioneshwa kusikitishwa na vitendo vya rushwa katika sekta ya ardhi nchini Naibu Waziri Pinda amesema ni lazima vyuo vya ardhi vianzishe mtaala wenye somo la maadili ndani yake ili wanachuo hao watakatakapoanza kuitumikia jamii wasiendelee na changamoto ya rushwa inayoigubika sekta hiyo.

Naibu Waziri Pinda amesema hayo leo wakati wa Mahafari ya 41 ya Chuo cha Ardhi Morogoro yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho nakuhudhuliwa na wahitimu takriban 300 waliofuzu katika fani mabalimbali za sekta ya ardhi.

‘’Inasikitisha kuona mwananchi anafuatilia hati mwaka mzima au mwananchi kwenda katika ngazi ya Wizara hadi Ikulu kufuatilia Migogoro wakati Wizara ina watumishi kuanzia ngazi ya Mikoa.’’Aliongeza Naibu Waziri Pinda.

Ameonya kuwa malalamiko ya Wananchi hayatakiwi kwenda kwa viongozi wa wajuu wa serikali kwani wao sio wataalamu wa ardhi masuala ya ardhi kwani changamoto hizo ni bora zikatatuliwa na wataalam wenye ujuzi katika fani hiyo.

Pinda ameagiza Wakurugenzi katika Wizara yake waangalie uwezekano wa kutumia wahitimu wapya sekta ya ardhi ili wapewe kazi katika miradi yote inayoendelea wizarani ili kuwajengea uwezo wa kufanyakazi kiufanisi mara watakapopata ajira rasmi.

Habari Zifananazo

Back to top button