Song afutwa kazi Cameroon

CAMEROON: Kocha Rigobert Song amefutwa kazi ya kuinoa timu ya Taifa ya Cameroon kutokana na mwenendo wa matokeo mabovu ndani ya kikosi hicho.

Song alibeba rasmi majukumu hayo mwaka 2022, alikuwa kwenye shinikizo kubwa hasa baada ya Cameroon kushindwa kufanya vyema katika michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2023 nchini Ivory Coast ambapo timu hiyo iliishia hatua ya 16 bora.

Shirikisho la mpira nchini Cameroon (FECAFOOT) chini ya Rais, Samuel Eto’o limeamua kumpiga chini nguli huyo wa kandanda kwenye taifa hilo baada ya kumalizika kwa kandarasi yake na sasa anasakwa mrithi wa kubeba mikoba hiyo.

Eto’o amenukuliwa akisema maaumizi ya kuachana na Song ni kwa ajili ya maslahi mapana ya timu ya taifa.

Rigobert Song akiwa na timu hiyo aliisaidia kufuzu fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Qatar mwaka 2022 hata hivyo Cameroon iliishia hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa ulimwenguni.

Katika michezo yake 23 ya mwisho na mabingwa hao mara tano wa michuano ya Mataifa ya Afrika Song aliibuka na ushindi katika michezo sita pekee.

 

Habari Zifananazo

Back to top button