Sopu: Nataka nimfunge tena Diarra

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Abdul Suleiman ‘Sopu’, amesema anatamani Yanga ishinde mchezo wa Nusu Fainali wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC), ili akakutane tena na kipa Djigui Diarra kwenye mechi ya fainali.

Akizungumza na HabariLEO, mshambuliaji huyo amesema anajua udhaifu wa kipa huyo ndio maana anatamani kukutana naye, ili aisaidie timu yake kubeba ubingwa.

“Diarra ni kipa mzuri lakini huwa sipati tabu kumfunga, najua upungufu wake na ndio huwa natumia kumfunga mara kwa mara,” amesema Sopu na kueleza kuwa anataka wakutane naye ili amfunge tena.

 

Katika mchezo wa Fainali ya Kombe la ASFC  msimu uliopita kati ya Coastal Union na Yanga, Sopu alifunga hat-trick, katika sare ya mabao 3-3, kabla ya Yanga kushinda Kwa mikwaju ya penalti.

Mchezo wa marudiano Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, kati ya Yanga na Azam, ambao Yanga ilishinda mabao 3-2, mabao ya Azam yalifungwa na Sopu.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button