Southampton yamfukuza kocha wao Ralph Hasenhüttl

KLABU ya Southampton imemfukuza kocha wao, Ralph Hasenhüttl kutokana na mwenendo usioridhisha baada ya jana kukubali kipigo cha mabao 4 -1 kutoka kwa New Castle United.

Hasenhuttl, ambaye aliteuliwa kuifundisha timu hiyo Disemba 2018, anaondoka katika klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya 18 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 14.

Southampton walishinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Bournemouth Oktoba 19, ambapo ulikuwa ushindi wao wa kwanza katika mchezo tisa iliyopita.

“Sasa tunaamini ni wakati wa mabadiliko,” imeeleza taarifa ya klabu hiyo. Sasa Ruben Selles atashika nafasi hiyo katika mchezo wa Carabao Cup raundi ya tatu dhidi ya Sheffield Wednesday utakaopigwa Jumatano hii.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x