Soya na maajabu yake kwa afya, kipato kwa mkulima

ANJELIKA Kitime ni mkulima wa soya katika Kijiji cha Mgama kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa. Anasema alianza kilimo cha soya mwaka 2017 kwa eneo la nusu ekari, baada ya hapo alilima ekari nzima na mwaka huu amelima ekari mbili.

Mkulima huyo anasema mwaka jana alitumia mbegu aina mbili ya Sipack na Uyole2, lakini mwaka huu aliitumia mbegu hiyo ya Sipack na Safari kwa kuhofia kusingekuwa na mvua ya kutosha lakini ikawa tofauti mvua zikanyesha. Anjelika pia ni mhudumu wa afya ya jamii.

Anasema kilimo cha soya kimemfanya atoe ushauri kwa wazazi kutumia lishe ya soya pindi anapomkuta mtoto ana uzito wa chini. Kuhusu kilimo hicho anasema alipoanza kulima nusu ekari alivuna gunia tatu, alipolima ekari moja alivuna gunia saba na mwaka huu amelima ekari mbili matarajio yake ni kupata gunia 14 zenye ujazo wa kilogramu 700.

“Ninapenda kulima mbegu aina ya Sipack kwa sababu inatoa mafuta mengi. Kilo 100 ya soya zinatoa mafuta lita 10,” anasema. Anjelika anakiri kupata mafanikio katika kilimo hicho kwa kuwa licha ya kuvuna soya na kutengeneza lishe ama kuuzia wenye viwanda, amekuwa akilima na kuuza mbegu. Mafanikio mengine ni kwamba amekuwa akiuza soya kilo Sh 1,500 mpaka Sh 3,000, lakini kwa kuwa wanunuzi hawachukui kidogokidogo huamua kuchakata soya kwa kuongezea thamani.

“Ninapovuna ninachakata mwenyewe ninatengeneza lishe na majani ya chai. Ukichakata mafuta kilo 100 za soya zinatoa mafuta lita 10, hivyo ninapata faida ya shilingi 450,000. Mafuta ninapata shilingi 300,000 na mashudu ninapata shilingi 150,000,” anasema.

Kwa maelezo yake soko la soya ni kubwa ila wakulima ni wachache, kinachotakiwa ni kuwahamasisha walime kwa wingi kwa kuwa soko lake ni kubwa na ina faida kubwa mwilini. Akielezea changamoto za zao hilo anasema zipo kwenye uvunaji na kupiga ili zipatikane soya.

Anjelika anasema mashine za kuvunia zipo ila kutokana na kipato alichonacho hawezi kumudu gharama ndio maana anapambana akitumia familia yake kuvuna. Soya ni zao muhimu kwa ajili ya lishe ya wanadamu na mifugo kwenye matumizi ya nyumbani na viwandani, kwani mafuta yaliyoko kwenye zao hilo ni asilimia 20 na protini asilimia 40.

Maeneo yanayofaa kwa kilimo cha soya nchini ni mengi ila mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa maharagwe, soya ni Ruvuma, Mbeya, Songwe, Njombe, Morogoro, Iringa na Rukwa. Mratibu wa Utafiti, Kilimo na Ubunifu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Kituo cha Ilonga kilichopo Kilosa mkoani Morogoro, Meshack Makenge ambaye pia ni Mratibu wa utafiti programu ya mazao jamii ya mikunde nchini anaelezea zao hilo kwa kina.

Makenge anasema Tari Ilonga hadi sasa kitaifa ina jukumu la kusimamia na kuratibu utafiti na uzalishaji wa mbegu za soya kikishirikiana na kituo cha Tari Uyole kilichopo mkoani Mbeya kwa lengo la kuhakikisha mbegu bora zinapatikana kwa wakulima nchini.

Makenge anasema mbegu zilizogunduliwa nchini zinazotumika na wakulima pamoja na wadau zipo aina 10 kati ya hizo aina tano zimegunduliwa na watafiti wa Tari zikiwemo Bossier, Uyole Soya 1, Uyole Soya 2, Uyole Soya 3 na Uyole Soya 4. “Zilizogunduliwa na kampuni za mbegu ni Sc Semeki, Sc Signal, Sc Saxon, Lundi na Mwenezi,” anasema Makenge. Kwa maelezo yake, Tanzania ina uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni mbili.

Na kwamba uzalishaji wa soya umeendelea kuongezeka kutoka tani 6,000 mwaka 2017 hadi tani 23,000 mwaka 2021. Vilevile maeneo ya uzalishaji yameendelea kukua kutoka hekta 7,000 mwaka 2010 hadi hekta 17,500 mwaka 2019.

Akizungumzia tija kwa wakulima, Makenge anasema bado ni ndogo kwani wanapata tani 0.7 hadi 0.9 kwa hekta ukilinganisha na uwezo wa mbegu bora zinazoweza kuzalisha tani 2.5 kwa hekta.

Akizungumzia changamoto zinazokabili zao hilo anasema ni za kiikolojia kwani mifumo ya kiteknolojia, upatikanaji mdogo wa mbegu bora husababisha kushindwa kufikia ubora wa nafaka ya soya.

Nyingine ni mitaji midogo kwa wadau wa mnyororo wa thamani, uwezeshwaji mdogo wa mafunzo kwa watafiti na wagani, miundombinu hafifu na matumizi machache ya fursa kwenye zao la soya kulinganisha na uhalisia wake.

Anasema matarajio ya Tari kwa kushirikiana na wadau nchini ni kuongeza utafiti wa mbegu bora zenye tija endelevu zinazoendana na mahitaji ya soko na mazingira ya uzalishaji na kutolea mfano uzaaji, usalama kiafya na lishe kufikika kirahisi na watumiaji.

“Tari inahakikisha upatikanaji mbegu zenye kubeba sifa inayohitajika sokoni. Pia inafanya tafiti za agronomia na masoko kukamilisha mnyororo wa thamani wa zao la soya nchini.

Kupitia utafiti huu tutakidhi mahitaji ya soya kwa soko la ndani na soko la nje kwa nchi za China, India na Falme za Uarabuni ambao wanahitaji soya kwa wingi. “Pato la taifa litaongezeka, usalama wa chakula utaimarika na umaskini nchini utapungua na wananchi watakuwa na maisha bora na kuwa na kipato cha kujikimu. Ajira zitaongezeka kupitia ujenzi wa viwanda vya kuchakata soya kwa ajili ya ukamuaji mafuta, utengenezaji wa vyakula vya mifugo na vya wanadamu,” anasema.

Pia anasema soya ni zao ambalo ni muhimu kwa ajili ya kukabiliana na utapiamlo. Watoto na wajawazito ni makundi yanayohitaji protini kwa wingi. “Kwa hiyo utaona zao hili ndilo linafaa sana kwa ajili ya lishe. Ukiachilia mbali protini asilimia 30 mpaka 46 pia linatoa mafuta ya kula kwa wingi,” anasema Makenge.

Anasema ni zao lililo katika mkataba na Wizara ya Kilimo kupeleka mbegu au nafaka nchini China. “China wanahitaji tani 103 za soya lakini Watanzania tunazalisha takribani tani 28 kwa hiyo tunahitaji kuzalisha kwa wingi soya kutosheleza soko la China,” anasema Makenge.

Soya ni zao linalolimwa nchini. Liligunduliwa nchini China kati ya miaka ya 2800 mpaka 2300 Kabla ya Kristo (BC). Mwishoni mwa miaka ya 1800 soya ilienea Pwani ya Afrika Mashariki. Iliingia Tanzania ikiletwa na Wajerumani mwaka 1907.

Baadaye mbegu ziliendelea kuingizwa nchini kutoka India, Afrika Kusini na Mashariki ya mbali. Ingawa maeneo yanayozalishwa mahindi, soya ikipandwa inaweza ikastawi vizuri kwenye maeneo hayo. Soya inahitaji mvua kiasi cha milimita 500 zenye mtawanyiko mzuri kwa muda wa miezi mitatu hadi minne.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Carolyn J. Thomas
Carolyn J. Thomas
2 months ago

I currently make about 6000-8000 dollars /month for freelancing I do from my home. For those of you who are ready to complete easy online jobs for 2-5 h every day from the comfort of your home and make a solid profit at the same time
.
.
Try this work______ http://www.pay.hiring9.com

Janice Goldman
Janice Goldman
Reply to  Carolyn J. Thomas
2 months ago

My last month paycheck was for 11000 dollars… All i did was simple online work from comfort at home for 3-4 hours/day that I got from this agency I discovered over the internet and they paid me for it 95 bucks every hour…. for more info visit any tab this site 
HERE====)> https://Www.Worksprofit.com

Elisabethappello
Elisabethappello
Reply to  Carolyn J. Thomas
2 months ago

Scam scam every where but don’t worry , every one is not a cheater, very reliable and profitable site. Thousands peoples are making good earning from it. For further detail visit the link no instant money required free signup and information…….__ https://onlineweb76.blogspot.com

Last edited 2 months ago by Elisabethappello
AlmaGreer
AlmaGreer
2 months ago

I am making $92 an hour working from home. i was greatly surprised at the same time as my neighbour advised me she changed into averaging $ninety five however I see the way it works now. I experience mass freedom now that I’m my non-public boss. 

That is what I do………….>>> https://excellentwork05.blogspot.com

Last edited 2 months ago by AlmaGreer
Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x