Spika: Serikali ifanye tathimini uagizaji mafuta
DODOMA; SPIKA wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametaka ifanyike tathmini ya mfumo mpya wa uagizaji mafuta nchini.
Ametoa kauli hiyo bungeni muda mfupi kabla ya kusitisha shughuli za bunge mchana leo Septemba 7, 2023 na kusema ni wakati mwafaka kwa serikali kufanya tathimini kwa mfumo huo wa uagizaji mafuta kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza.
Amesema haiwezekani mafuta yanapatikana kwa wiki mbili na baada ya hapo yanakuwa hayapatikani, kisha baada ya muda yananza kupatikana.
Amesema kama mfumo huo unaleta changamoto basi warejee katika mfumo wa zamani kwa kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto, lakini kama mfumo wa sasa nao unaonekana ni sahihi basi waangalie maeneo yenye changamoto parekebishwe.