Spika: Vijana pigeni vita matamshi ya chuki

Spika: Vijana pigeni vita matamshi ya chuki

SPIKA wa Bunge, Donatille Mukabalisa amewataka vijana kupiga vita kauli za chuki na uchochezi ili kujenga amani na umoja endelevu.

Akizungumza katika mdahalo wa wabunge wa vijana ulioandaliwa na Wizara ya Umoja wa Kitaifa na Ushirikiano wa Kiraia (MINUBUMWE) inayofanya kazi pamoja na Never Again Rwanda (NAR) na washirika, alisema umoja wa Wanyarwanda ndio nguvu ya taifa lao.

Mdahalo huo uliofanyika sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani inayoadhimishwa Septemba 21 kila mwaka, uliwakutanisha washiriki zaidi ya 500 wakiwemo vijana kutoka wilaya mbalimbali.

Advertisement

Wengine walioshiriki katika mdahalo huo ni pamoja na wabunge, watendaji wa kujenga amani, watunga sera na washirika wa maendeleo.

Mdahalo huo pamoja na mambo mengine, ulilenga kujadili mikakati na mbinu za kudumisha umoja hasa vijana wanapokabiliana na matamshi ya chuki kwa njia tofauti kama kikwazo kwa umoja wa Rwanda.

Mukabalisa aliwatahadharisha vijana dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa kuwa mara nyingi hutumiwa pia na watu wanaoitumia kuungwa mkono na watu wasioitakia mema nchi.

“Amani na usalama tuliopigania umekuwa nguzo ya maendeleo tunayoadhimisha leo…. Safari bado ndefu kwa sababu Wanyarwanda, bado tuna malengo mengi ya kufikia na hatuwezi kuyafikia bila kufanya kazi pamoja,” alisema.

Waziri wa Umoja wa Kitaifa na Ushirikiano wa Kiraia, Jean-Damascene Bizimana, aliwataka vijana kutowaogopa wanaopandikiza chuki na migogoro.

“Historia ya kusikitisha ambayo nchi yetu imepitia lazima iwape msukumo vijana katika kuunganisha juhudi na kurekebisha makosa ya nyuma. Serikali iko tayari kuunga mkono, kuwa kielelezo chako, kutoa usalama na kufanya kazi na wewe kuendeleza amani.”

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Never Again Rwanda, Eric Mahoro aliupongeza uongozi wa nchi hiyo kwa kuendelea kuwaamini vijana, kuwasikiliza na kuwaonesha njia ya kuelekea kwenye amani endelevu.

 

 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *